JUMA LA MAOMBI TUCASA STUM ALIHAMISI SOMO HILI NI MBARAKA SANA

Thursday, May 25, 2017 SOMO: SIKU DUNIA ITAKAPOSIMAMA. Mwandaaji: Clinton Omuyanja, Mwenyekiti Msaidizi wa Union Fungu kuu: Yoshua 10:12,13. Mathayo 27:45-53. Wimbo namba 107 kitabu kidogo. Je, umewahi kusikia dunia iliwahi kusimama. Wataalamu wa jiografia wanadai kuwa, dunia inapozunguka katika mhimili wake tunapata usiku na mchana. Dai hili si kweli kwa kuwa tangu mwanzo Mungu aliumba nuru na giza, nayo nuru ikatawala mchana na giza usiku [Mwanzo 1:4,5,16]. Ni kweli kuwa dunia imewahi kusimama zaidi ya mara moja katika historia. Dunia ilisimama wakati Yoshua akikabiliana na majeshi ya wafalme watano waliokwea dhidi yake na wana wa Israeli. Kwa ajili ya maombi ambayo Yoshua alimwomba Mungu, Dunia ilisimama kwa kuwa jua liliposimama haukuwa utaratibu wa kawaida kwa dunia. Leo vijana tulioitwa na Kristo tunaitazama dunia ambayo inaenda kwa mwendo unaoelezwa na Isaya 24:19 kuwa dunia inayumba yu...