JUMA LA MAOMBI TAR 21/5 LA TUCASA STUM
Mpendwa mtembeleaji wa blogg hii nimekuwekea juma la maombi
Sunday, May 21, 2017SOMO: ONGOA ROHO MOJA, SHIRIKI KUUBADILISHA ULIMWENGU.Mwandaaji: ESTHER MAYUNGA, MHAZINI MKUU ETC
Fungu kuu: Marko 16:15. Wimbo namba 107 kitabu kidogo.Bwana ametuita kuubadilisha ulimwengu kwa kuokoa wengine. Ni kazi ya pekee
ambayo malaika hutamani kuifanya lakini Bwana ameiacha mikononi mwetu kwa ajili ya
ukombozi wa maisha yetu. Mpendwa, katika mwaka 2017/2018 wa utendaji
umejiaandaaje kushiriki katika kuubadilisha ulimwengu kwa kuokoa wengine ambao
hawajamjua Mungu wa pekee na wa kweli.
Kwa kutambua kusudi la kuokolewa kwake, mtume Paulo anasema, “Ya kuwa
sikujiepusha katika kumtangazia neno lolote liwezalo kufaa, bali naliwafundisha
waziwazi na nyumba kwa nyumba [Matendo 20:20]’ Kazi ya kupeleka Neno la Mungu
kwa kila mlango wa mtu na kutafuta kwa ajili ya Kristo roho zinazoangamia kwa kukosa
ukweli ni ya muhimu na inahitajika sasa. Katika kipindi hiki ambapo muda si mrefu
historia ya ulimwengu itafungwa, Bwana ametuagiza wanaume na wanawake, na
wazee kwa vijana kwenda ulimwenguni na kuihubiri injili kwa kila kiumbe [Marko 16:15].
Kabla na baada ya Yesu kusema, ‘Enendeni’. Aliahidi uwezo, kwanza ‘uwezo wote’
kutoka kwenye Kiti cha enzi. Pili kuwako kwake, hapa mpaka mwisho [Biblia Ya Sema
uk,97]. ‘Sisi sote tu wajumbe wa KRISTO. “Maana Mungu alikuwa ndani ya Kristo
akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake naye ametia neno la upatanisho ndani yake.
Baba wa Mbinguni leo anasihi kupitia maisha yetu, tuweze kuupatanisha ulimwengu na
Mungu kwa ajili ya Kristo [2 Kor 5:19,20].
‘Ujumbe wa malaika wa tatu ambao ni ujumbe wa kuhesabiwa haki kwa imani katika
Kristo Yesu, Kristo ni haki yetu. Ni muhimu kiasi gani basi kwa watu wa Mungu
kujifunza kwa bidii ukweli huu na kuuishi kwa ajili ya wokovu wetu wenyewe na pia kwa
ajili ya wokovu wa wale tunaotakiwa kuwapelekea ukweli huu wa leo. [Ujumbe wa
Mwisho uk. 161, 162].
Tumeokolewa ili kuokoa wengine. Wale wote walio tayari kutumika kwa kazi ya Bwana
pasipo kujali udhaifu wao, Bwana atawafundisha jinsi ya kuenenda kwa ujasiri wa
SOMO LA JUMA LA MAOMBI: MAY 21-27, 2017 TUCASA STUM
imani. Atawafanya wawe imara kwa kuunganisha udhaifu wao katika nguvu zake.
Atawafanya kuwa na hekima kwa kuunganisha kutokujua kwao na hekima yake
[Mapambano na Faraja sehemu ya kwanza uk 123].’ Leo kama mtaisikia sauti yake
msifanye migumu mioyo yenu.’
Kupitia utume wa nyumba kwa nyumba, mihadhara ya neno la Mungu, michango,
maombi na mwenendo safi wa kila mmoja katika kipindi hiki cha ushirikishwaji wa kila
mwana TUCASA. Tumia muda wako kuubadili ulimwengu kwa Neno la Mungu maana
BWANA amekuokoa ili uokoe wengine. Weka mpango wa kuleta angalau roho moja
kwa Kristo katika mwaka huu wa masomo.
Mambo ya Kuombea:
1. Uinjilisti – Kila Mwanachama kuleta Roho moja kwa Kristo katika mwaka2017/18.
2. Roho Mtakatifu na Mafanikio ya Global PCM Weekend
3. Viongozi wa TUCASA katika ngazi zote.
4. Umoja, Upendo na Ushirikiano katika TUCASA
5. Mungu atusaidie tuweze kumpenda, kulipenda neno Lake na kipenda kazi yake.
6. Mambo mengine kadri Bwana atakavyowaongoza
Comments
Post a Comment