JUMA LA MAOMBI TUCASA STUM ALIHAMISI SOMO HILI NI MBARAKA SANA
Thursday, May 25, 2017SOMO: SIKU DUNIA ITAKAPOSIMAMA.Mwandaaji: Clinton Omuyanja, Mwenyekiti Msaidizi wa Union
Fungu kuu: Yoshua 10:12,13. Mathayo 27:45-53. Wimbo namba 107 kitabu kidogo.
Je, umewahi kusikia dunia iliwahi kusimama. Wataalamu wa jiografia wanadai kuwa,
dunia inapozunguka katika mhimili wake tunapata usiku na mchana. Dai hili si kweli kwa
kuwa tangu mwanzo Mungu aliumba nuru na giza, nayo nuru ikatawala mchana na giza
usiku [Mwanzo 1:4,5,16].
Ni kweli kuwa dunia imewahi kusimama zaidi ya mara moja katika historia. Dunia
ilisimama wakati Yoshua akikabiliana na majeshi ya wafalme watano waliokwea dhidi
yake na wana wa Israeli. Kwa ajili ya maombi ambayo Yoshua alimwomba Mungu,
Dunia ilisimama kwa kuwa jua liliposimama haukuwa utaratibu wa kawaida kwa dunia.
Leo vijana tulioitwa na Kristo tunaitazama dunia ambayo inaenda kwa mwendo
unaoelezwa na Isaya 24:19 kuwa dunia inayumba yumba, yamkini tunaiona kuwa
mahali salama tukisahau miito yetu katika maombi na sala nakutenda kazi kwa kujitoa
mioyo yetu katika shamba la Bwana.Ipo siku moja dunia itasimama.
SOMO LA JUMA LA MAOMBI: MAY 21-27, 2017 TUCASA STUM
Tena dunia ilisimama siku Yesu alipotoa sadaka ya uhai wake kwa ajili ya wanadamu
wote. Siku hiyo aliposulubiwa, hatimaye alikata roho, mara dunia ikasimama kukawa na
giza tangu saa sita hadi saa tisa. Ni takribani masaa matatu dunia ilishindwa kuvum ilia
pale Kristo alipokata roho. Dunia haikustahimili kuwa katika namna yake ya kawaida.
Hapo dunia iliposimama nchi ilitetemeka, miamba ilipasuka, makaburi yakafunuka, na
ikanuka miili ya wafu waliolala. Mathayo 27:45-53.
Ndipo tunapopewa tangazo kuwa iko siku dunia itakaposimama. Je ni siku ipi? Hakika
ni siku Yesu atakaporudi, siku hiyo dunia itasimama tena. Matukio kama yale
yaliyotokea wakati wa mauti ya Yesu yatatokea tena nayo ni ufufuo wa wafu waliolala
katika mavumbi ya nchi na haitaweza kusitahimili ujio huu wa Masihi.
Swali muhimu la kutafakari ni hili, wakati dunia itakaposimama tutakuwa tukiendelea
kuishi kwa namna inayotupendeza sisi wenyewe? Bila shaka kila mmoja wetu
angetamani kuwa mmoja kati ya hao watakaomtukaza Mungu wakati dunia
itakaposimama. Wako wapi vijana watakao simama kumtetea Kristo wakati dunia
inapoelekea Ukingoni? Ni akina nani watakao simama mahali pa Yoshua dunia
inaposimama?
Ujumbe; Yeye aliyeiumba dunia na kuisimamisha wakati wa mauti yake atarudi tena na
kuisimamisha dunia. Hivyo tunapaswa kusimama upande wake wakati Dunia
inaposimama.
Wito: Tunaalikwa kujitoa kikamilifu kwa Mungu, ili atujaze Roho wake huku tukifanywa
tayari kuwa kama Yoshua aliyemtegemea Mungu hata ikawa alipoomba akasimamisha
jua na dunia ikasimama. Ungana na wana TUCASA katika union ya kusini mwa
Tanzania kuleta angalau roho moja kwa Kristo katika mwaka huu wa masomo.
Mambo ya Kuombea:
1. Uinjilisti – Kila mwanachama kuleta roho moja kwa Kristo katika mwaka 2017/18.
2. Roho Mtakatifu na mafanikio ya Global PCM Weekend
3. Mfanikio ya SUMMIT ya 2018 – Wahudumu, mahudhurio na Uongozi wa Bwana
katika kila jambo.
4. Kwaya za TUCASA – Mtindo wa maisha, mipango na roho ya uinjilisti iwe juu
yao.
SOMO LA JUMA LA MAOMBI: MAY 21-27, 2017 TUCASA STUM
5. Machaplain na walezi wetu.
6. Mambo mengine kadri Bwana atakavyowaongoza.
Comments
Post a Comment