JUMA LA MAOMBI TUCASA STUM
SOMO LA PILI
Tuesday, May 23, 2017
SOMO: MTAZAMO, MSIMAMO NA MAONO YATAKAYO BADILI ULIMWENGU KWA
WAKATI KAMA HUU.
Mwandaaji: Karangi Joel, Mwenyekiti wa TUCASA ETC
SOMO LA JUMA LA MAOMBI: MAY 21-27, 2017 TUCASA STUM
Fungu kuu: Mwanzo 32:24-26. Wimbo namba 107 kitabu kidogo.
Changamoto za sasa za kimaisha, kielimu, kiuchumi na kijamii wanazokumbana nazo
vijana wakike na wakiume zimekua chachu kubwa kwa vijana kukata tamaa ya maisha
na kurudi nyuma katika maisha yao ya kiroho. Mipango ya maisha ya baadae ambayo
vijana wamekuwa wakijiwekea na ndoto ambazo wamekua wakizitazamia zitimie katika
maisha yao zimekuwa zikipotea pale tu changamoto zinapo wakabili nawao kushindwa
kukabiliananazo.
Hali hii imewafanya vijana wengi hasa wanafunzi na wale wasio wanafunzi ambao
wamekutana na nyakati tofauti kama hizi katika maisha kuchukua maamuzi yasiyo
sahihi. Maamuzi hayo yamepelekea kudumbukia katika dimbwi zito la kimaaamuzi, na
maamuzi hayo kusababisha matokeo hasi katika maisha. Miongoni mwa hayo ni
matumizi ya madawa ya kulevya, msongo wa mawazo na hata kujinyonga. Haya
yamekuwa ni matukio ya kawaida na yakusikitisha kabisa yanayo kabili jamii ya vijana
wanao mwamini Kristo na hata wale wasio amini.
Kijana Yakobo kwa muda wa miaka 20, alikutana na chanagamoto nzito zilizompelekea
kukaa katika njiapanda ya kimaamuzi.
1
Kuhusu kukwapua baraka za kaka yake Esau
na kuondoka kwa mjomba wake Labani pasipokuaga, akiwa katikati ya pori amekosa
uelekeo, ulikuwa ni wakati muhimu wa kupima maamuzi sahihi ya Yakobo. (Mwanzo
31:22, 23)
Katika dimbwi la kukata tamaa, dimbwi la upweke, dimbwi la kufeli ndio wakati wa
kusimama imara kama vijana kuyakita maisha yetu kwa Kristo. Kuyakabidhi maisha
yetu kwake ndiyo njia pekee ya kuubadili ulimwengu katika nyanja zote za changamoto.
Ndani ya hili juma la mibaraka na kujiweka wakfu hebu natung’ang’anie ulinzi wa Kristo
pasipo kulegea. (Mwanzo 4:24-26) Maisha ya Yakobo kama kijana wa kipindi hicho
yakawe chachu na mfano wa kusonga mbele katika kumtumaini Mungu na pia katika
utumishi.
Pale Yakobo alipokuwa na wasiwasi mkubwa juu ya hatima ya maisha yake, dhidi ya
kaka yake Esau, (Mwanzo 33:1) na pale mjomba wake Labani alipo mgeuka (Mwanzo
1
Spirit of Prophecy Vol.1 page 122-124
Comments
Post a Comment