ENDELEA KUBALIKIWA Wednesday, May 24, 2017 SOMO: UTUME NI WETU SOTE. Mwandaaji: Maregesi January Simula, Mwenyekiti TUCASA SEC 2017/18 Fungu kuu: Mathayo 28:19, 20. Wimbo namba 107 kitabu kidogo. SOMO LA JUMA LA MAOMBI: MAY 21-27, 2017 TUCASA STUM Baada ya kufa kwa Mwokozi wanafunzi walikata tamaa sana na kufa moyo. Jua la matumaini katika mioyo yao lilikuwa limekuchwa, na giza ndilo liliwafunika. Waliyakumbuka maneno ya Kristo wakiwa katika hali ya ukiwa na upweke kabisa. Maneno ya Kristo yalisema hivi; “Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?” Luka 23:31 Wanafunzi hali wakijawa na huzuni na majonzi wakiwaza sana kwamba ikiwa Yesu waliyemwamini na kumtegemea amefanyiwa hivyo wao je, ni nini kitakachowapata wao? Kwa hofu hiyo walikusanyika katika chumba cha juu, wakafunga milango, wakiogopa wasipatwe na mambo yaliyompata Yesu. Hapa ndipo Mwokozi alipokutana nao baada ya kuf...
KONA YA INJILI KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO LINAWALETEA MASOMO YA JUMA LA MAOMBI KW VIJANA WAKUBWA USIPITWE KUANZIA TAREHE 19-25/03/2017 NIJUZE KANISANI KWAKO KUMEKUAJE NA JE VIJANA WANAITIKIA WITO HUU USIKOSE!!!! KUPATA TAARIFA MBALIMBALI ZA INJILI NA MAMBO MENGINE YA KIJAMII T BLOG HIII
TUCASA CHUO KIKUU MZUMBE WAKEINDESHA MIKUTANO YA INJILI KATIKA ENEO LA VITONGA Tangu tarehe 4-marchi hadi tarehe 17-marchi 2018 vijana hawa watakua katika eneo la vitonga kwa ajili ya kutangaza habari nema za matumaini ambapo asomo mbalimbali yatakua yakitolewa na kuletwa mubashara kabisa kutakua n msomo yafuatayo 1:UJASIRIAMALI 2:AFYA 3:MASOMO YA NDOA 4:NENO LA MUNGU 5:MIANZO MIPYA NA MJUE MUNGU SERIES masomo haya yataletwa na yanatolewa na watumishi wa MUNGU Mr KELVIN (Ujasiriamali) Ev: PATRICK AYOUB (Afya) Pr: SULEIMANI(Ndoa) Pr: ISACK NKYA(Neno la MUNGU) Ev: MUYENGI BS Jr(Mianzo mipya na Mjue MUNGU series) Nyote mnakaribishwa na kwa sababu hiyo MUYENGI ONE NIJUZE tutakua tunakusogezea habari hizi endelea kufuatana nasi ubarikiwe
Comments
Post a Comment