ENDELEA KUBALIKIWA Wednesday, May 24, 2017 SOMO: UTUME NI WETU SOTE. Mwandaaji: Maregesi January Simula, Mwenyekiti TUCASA SEC 2017/18 Fungu kuu: Mathayo 28:19, 20. Wimbo namba 107 kitabu kidogo. SOMO LA JUMA LA MAOMBI: MAY 21-27, 2017 TUCASA STUM Baada ya kufa kwa Mwokozi wanafunzi walikata tamaa sana na kufa moyo. Jua la matumaini katika mioyo yao lilikuwa limekuchwa, na giza ndilo liliwafunika. Waliyakumbuka maneno ya Kristo wakiwa katika hali ya ukiwa na upweke kabisa. Maneno ya Kristo yalisema hivi; “Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?” Luka 23:31 Wanafunzi hali wakijawa na huzuni na majonzi wakiwaza sana kwamba ikiwa Yesu waliyemwamini na kumtegemea amefanyiwa hivyo wao je, ni nini kitakachowapata wao? Kwa hofu hiyo walikusanyika katika chumba cha juu, wakafunga milango, wakiogopa wasipatwe na mambo yaliyompata Yesu. Hapa ndipo Mwokozi alipokutana nao baada ya kuf...
Comments
Post a Comment